MAKALA : IFAHAMU SWANSEA FC TIMU KUTOKA NJE YA ENGLAND INAYOWANYIMA RAHA WENYEJI



MAKALA : IFAHAMU SWANSEA FC TIMU KUTOKA NJE YA ENGLAND INAYOWANYIMA RAHA WENYEJI

SWAN

As Monaco ni miongoni mwa timu chache barani Ulaya ambazo zinashiriki ligi za nchi nyingine. Nafahamu binadamu wengi hasa Waafrika ni wavivu kusoma na hamfahamu kuwa Monaco ni jimbo ambalo linajitegemea kama nchi na siyo sehemu ya Ufaransa. Siku sio nyingi tutaziingiza Fc Barcelona na Espanyol kwenye kundi hili kwani Jimbo la Cataluna linapigania ukombozi wa kujitenga. Kwa maana hiyo La liga watazikaribisha timu hizi kama ambavyo As Monaco na Swansea zinafanya kwenye ligi za French league 1 na Epl. Pia zipo timu nyingi zenye mfano huu naamini siku nyingine tutaandika juu ya suala hili kwa mapana.

Timu ya Swansea ni miongoni mwa timu kwenye kundi hili. Kumbuka maana ya neno hili ni 'Yange yange' hawa ni ndege ambao wanapatikana hata huku kwetu Afrika. Kutokana na kufanya vizuri kwa timu hii ambayo ilimaliza nafasi 8 ni vyema tutazame baadhi ya vitu ambavyo sio vibaya kuvijua dhidi ya timu hii ambayo inafahamika kwa jina la utani kama Jacks' ila pia siku hizi wanasoka wanaiita 'Swanselona' ikiwa inafananishwa na Fc Barcelona kutokana na pasi zake uwanjani. Hapa chini baadhi ya vitu hivo….

Swansea city ndio timu ya kwanza kutoka nchi ya Wales kucheza Premier league baada ya kupanda daraja msimu wa 2010/12, huku Sinclair
akifunga magoli matatu katika mechi ya fainal. Cardiff city pia ilikuwa timu ya pili kucheza Epl msimu uliofuata licha ya kushuka daraja. Cardiff ni mji mkubwa ukifuatiwa na Swansea nchini Wales.

Swansea city ni miongoni mwa timu 6 ambazo zipo nchini Wales lakini zinayo nafasi ya kushiriki ligi kuu ya England. Hali hii ilitokea
baada ya timu hizi kukataa ofa ya kushiriki ligi kuu ya Wales kwani wamekuwa wakishiriki kwenye michuano inayoandaliwa na Fa tangu timu hizi zianzishwe ikiwemo ligi kuu ya Uingereza. Kumbuka ligi kuu ya Wales ilianzishwa mwaka 1992.

Jina la Swansea city lilizaliwa mwaka 1970 mara baada ya mji wa Swansea kupewa hadhi ya jiji, kabla ya hapo timu hii ilikuwa inajulikana kama Swansea town. Jiji hili ni miongoni mwa miji 20 mikubwa kabisa katika visiwa vya Uingereza.

Vetch Field ndio uwanja uliokuwa unatumiwa na Swansea, uwanja huu umetumika kwa miaka 93, tangu 2005 Swansea ilianza kuutumia Libertystadium. Vetch field ni uwanja ambao ulipewa jina hilo kutokana na mboga za majani kuota sana katika 'Pitch' ya uwanja huo.

Swansea imechukua kombe la Wales mara 10, walifanya hivo mara ya kwanza 1913, mara ya mwisho ilikuwa 1990. Wales cup ndio kombe kongwe na lenye heshima kubwa nchini Wales kama ilivyo kwa Fa nchini England. Kumbuka kwa sasa Swansea na timu zingine 6 haziruhusiwi kushiriki kikombe hiki tangu 1996 kutokana na kupewa nafasi ya kushiriki kombe la Fa.

Katika historia ya timu hiyo ushindi mkubwa kuwahi kuupata ni ule dhidi ya timu ya ligi kuu ya Malta, Sliema Wanderers kwenye kombe la
washindi ampapo kwa sasa linajulikana kama Uefa Europe league. swansea ilishinda 12-0 kwenye raundi ya kwanza msimu wa 1982 ambao ndio ulikuwa msimu wenye mafanikio makubwa kwenye timu hii. Swansea walitolewa na Napoli miaka ya hivi karibuni kwenye michuano hii.

Wakati Ryan Giggs wa Manchester United anashikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi klabuni kwa kucheza mechi 963, Roger Freestone ndiye mchezaji anaekumbuka zaidi kwa kucheza mechi nyingi, tangu 1989-2004 amecheza mechi 699. Huyu ni mlinda mlango na mpiga penati maarufu wa Wales aliyecheza kwa mafanikio, kwa wale wanaopenda kuziangalia timu za Wales, huyu jamaa alishawahi kukaa kwenye benchi la Swansea kama Kocha msaidizi.

Swansea ni timu ambayo huwa haifungi magoli mengi kwani hadi sasa Mchezaji wao Cyril Pearce rekodi yake ya kufunga magoli  35 msimu wa 1931/32 ndiyo ya juu na haijawahi kuvunjwa hata baada ya kuja kwa Wilfred Bony miaka ya hivi karibuni.

Cardiff city ndio wapinzani wao wakubwa, pindi timu hizi zinapokutana huwa mechi yao inaitwa 'South wales derby'. Hii ni miongoni mwa
'Derby' kubwa sana katika visiwa vya Uingereza. Kuna wakati mwamuzi Mike Dean alijeruhiwa vibaya baada ya kupigwa na mashabiki kwenye 'derby' hii ambayo ni gumzo sana nchini Wales.

Mchezaji raia wa Ivory Coast ambaye hivi karibu alionekana kwenye mtandao wa kijamii 'instagram' akikata mauno pale alipokuwa anacheza wimbo wa 'nasema nao' wa msanii wa Kitanzania Diamond-Platnum, ndiye anashikilia rekodi ya kununuliwa na kuuzwa kwa pesa nyingi katika klabu hiyo. Bony alisajiliwa kwa £12 Million kutoka Vitesse na kuuzwa
kwa £28  million kwenda Man city.

Mwaka 2013 ndio mwaka wa mafanikio ya karibuni kwa timu ya Swansea baada ya kushinda kombe la ligi kwa kuitoa timu ya Ki ingereza ya
Bradford city kwenye fainali iliyopigwa Wembley. Kumbuka michuano hii inajumuisha jumla ya timu 92 kutoka Wales na England, Swansea
iliwafunga Liverpool kwenye raundi ya 4.

Swansea ni timu ya wanachama, 20% ya hisa zake zinamilikiwa na wanachama wa timu hiyo na huwa wanajumuishwa kwenye mambo mbalimbali ya uendeshaji wa klabu. Diego Costa mpaka sasa anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji aliyewafunga Swansea magoli mengi. Diego amefunga magoli 5 hadi sasa katika mechi 3 alizocheza dhidi ya Swansea.

Andrew Ayew na Bafetimbi Gomez ni wachezaji weusi kuipatia Swansea pointi kwenye uwanja wa Stanford Bridge baada ya miaka 35. Swansea ilitoka sare ya magoli 2-2 na timu ya Chelsea wikiendi iliyopita. Msimu uliopita Swansea ilipata penati 2 pekee kwenye mechi zote na kuwa timu iliyopata penati chache kuliko timu zingine

By Salym Juma



Comments