Kocha wa Simba Dylan Kerr (katikati) akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kuifungia goli timu ya viongozi wa Simba
Kocha mkuu wa Simba Dylan Kerr jana alitupia goli pekee wakati timu ya viongozi wa Simba ilipoikabili timu ya Bongo Movies kwenye mchezo wa utangulizi kabla ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Simba SC dhidi ya SC Villa ya Uganda wakati wa maadhimisho ya siku ya Simba Day siku ambayo huadhimishwa kila ifikapo Agosti 8, kila mwaka.
Kerr alionesha bado yuko fiti kwenye mchezo huo kutokana na uwezo mkubwa aliounesha wakati akisakata kandanda uwanjani na kuwasumbua wachezaji wa Bongo Movies.
Licha ya kuwa kocha, Kerr aliwahi kucheza kama mlinzi wa kushoto kwenye vilabu tofauti vikubwa vya nchini England kama Sheffield Wednesday, Leeds United, Reading, Blackpool na vingine vingi kabla hajaanza rasmi kazi ya ukocha.
Kikosi cha wachezaji wa timu ya viongozi wa Simba pamoja na viongozi wengine wa benchi la ufundi wa kikosi hicho
Picha nyingine wakati wa mechi ya viongozi wa Simba SC dhidi ya Bongo Movies
Mchezaji wa timu ya viongozi wa Simba Ibrahim Masoud 'Maetro' akipasha misuli kabla ya kuingia uwanjani
Comments
Post a Comment