KOCHA MPYA WA JANG’OMBE BOYS ATUA ZANZIBAR TAYARI KUANZA KAZI


KOCHA MPYA WA JANG'OMBE BOYS ATUA ZANZIBAR TAYARI KUANZA KAZI
Memik Vurucu (kulia) kocha mpya wa Jang'ombe Boys baada              ya kutua visiwani Zanzibar

Memik Vurucu (watatu kutoka kulia) kocha mpya wa Jang'ombe Boys baada ya kutua visiwani Zanzibar

Furaha ya kupita kiasi leo hii ilikuwepo kwa wana jangombe boys, ambapo wamempokea kocha wao bandarini Zanzibar saa nane mchana akitokea nchini uturuki.

Kocha huyo mturuki anaitwa Memik Vurucu, ambapo amefurahishwa na mapokezi ya timu yake hiyo mpya.

Kama kawaida yake mtandao wa Shafiih Dauda ulifika kwenye mapokezi ya kocha huyo bandarini unguja na ukafanikiwa kuzungumza nae ambapo kwa mara ya kwanza akifika kwenye visiwa vya Zanzibar.

Memik Vurucu, amesema amefurahishi sana kufika visiwani Zanzibar lakini hakutaka kuzungumza sana na kusema zaidi ataongea baadae.

Mashabiki wa Jang'ombe Boys waliojitokeza kumpokea              kocha wao mpya wakati akiwasili Zanzibar

Mashabiki wa Jang'ombe Boys waliojitokeza kumpokea kocha wao mpya wakati akiwasili Zanzibar

Kwa upande wake rais wa timu hiyo Ali Othman amesema, "tumefurahi sana kwa ujio wa Kocha huyu, na naamini tutafanya vizuri katika ligi kuu ya Zanzibar msimu ujao".

Baada ya kupokewa kocha huyo, msafara ukapita barabara ya Malindi bandarini, Mlandege, Kisonge round about, njia ya Golf makaburini, wakatokea uwanja wa Tumbaku, wakapita round about ndogo ya Miembeni, wakapandisha barabara ya Matarumbeta kwa Baja, wakatokea Jang'ombe Mzizima, mwisho walipofika Jangombe gengeni, wakaingia ndani ya makao makuu ya Jang'ombe Boys ambapo kunajulikana kwa jina la fainali.

Kocha akakaribishwa na wazee wa mtaa wa Jang'ombe pamoja na wadau wote wa timu hiyo.

Kwa upande wake Issa Amasha ambae ndiye kocha aliyeipandisha ligi kuu timu hiyo amesema amefurahishwa na ujio wa kocha huyo ambapo alisema kuwa, yeye atajifunza lugha ya kituruki.

picha boys 3

Na kwa upande wao mashabiki wa Jang'ombe Boys wamefurahi kutokana ujio wa kocha huyo mturuki ambapo kila mmoja akisema kuwa wameweka historia mpya na wanaamini watafanya vizuri kwenye ligi kuu ya Zanzibar. Kocha Memik Vurucu amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia timu ya Jang'ombe Boys ambayo imepanda ligi kuu ya Zanzibar kwa msimu huu.



Comments