KASHFA NZITO: MPENZI WA ZAMANI WA DAKTARI WA CHELSEA EVA CARNEIRO AVUJISHA STORI YA AIBU….


KASHFA NZITO: MPENZI WA ZAMANI WA DAKTARI WA CHELSEA EVA CARNEIRO AVUJISHA STORI YA AIBU….
Screen-Shot-2015-08-16-at-9.51.41-AM
Gazeti la The Sun limekamilisha udaku wake na leo limekuja na kichwa cha habari kikisema kwamba daktari wa Chelsea, Eva Carneiro anawatumia vibaya wachezaji wa klabu hiyo.
Stori hii imekuja wiki ya kwanza tu baada ya Carneiro kushambuliwa hadharani na kocha Jose Mourinho kufuatia kuingia uwanjani kumtibu Eden Hazard wakati wa dakika za mwisho za mechi ambayo Chelsea walitoka sare ya 2-2 na Swansea City.
Matokeo yake, Carneiro amepunguziwa majukumu katika benchi la matabibu la Chelsea.
The Sun wamemshambulia Daktari huyo mwenye heshima kubwa kuwa ana mahusiano ya mapenzi na baadhi ya wachezaji wa Chelsea.
Mpenzi wa zamani wa Eva, Rupert Patterson-Ward, ndiye amevujisha taarifa hiyo kwa gazeti hilo akidai kwamba daktari huyo analala na moja ya wachezaji wa klabu hiyo, ingawa hajataja jina lake.
Eva Carneiro had an affair with a Chelsea player, says              doctors ex [Sun]
Nukuu hii hapa:
 
"Mwanamke huyu aliharibu maisha yangu. Eva angeweza kuniambi kwamba analala na moja ya wachezaji wa Chelsea, lakini alijua ningejisikia vibaya. Pia huenda alidhani siwezi kuamini.
Eva anajivunia sana kuwa maarufu miongoni mwa wachezaji. Anapenda sana kusifiwa".
"Eva ni mwanamke mwenye mvuto na watu wengi hawajui. Ana ushawishi mkubwa, anaweza kupata kila anachohitaji. Nilikaa naye katika mahusiano na tulipanga kuwa na familia, lakini aliniumiza na kunimwaga".
"Eva anapenda sana kufanya mapenzi. Mapenzi ni muhimu sana kwake. Tulikuwa tunafanya mapenzi kila siku".
Sio kwamba Rupert Patterson-Ward amewapa tu stori hiyo ya aibu, jamaa amevujisha mpaka picha zinazothibitisha kwamba wawili hao walikuwa wapenzi.
Eva Carneiro had an affair with a Chelsea player, says              doctors ex [Sun]
Eva Carneiro had an affair with a Chelsea player, says              doctors ex [Sun]


Comments