HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED



HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED
Screen-Shot-2015-08-16-at-00.46.19
Bayern Munich walianza vyema kutetea ubingwa wao wa Bundesliga wakiifunga 5-0 Hamburg SV kwenye mechi iliyopigwa Ijumaa iliyopita  uwanja wa Allianz Arena,  huku Thomas Muller akifunga magoli mawili.
Wakati huo huo, Manchester United walipata ushindi wao wa pili  kwa kushinda 1-0 dhidi ya Aston Villa, ingawa bado hofu ipo  katika safu yake ya ushambuliaji.
Leo gazeti la The Sunday Express limeandika stori ukurasa wake wa nyuma akisomeka: "Thomas Muller anataka kujiunga na Manchester United,  hii ni kwa mujibu wa John Richardson.
Sunday Express wanaonekana kupata habari hiyo kutoka vyanzo makini vya masuala ya usajili vinavyodai Muller anataka kujiunga na mchezaji mwenzake wa zamani wa Bayern Munich aliyetimkia Old Trafford,  Bastian Schweinsteiger.
Hata hivyo, bosi wa Man United, Louis van Gaal bado hajakata tamaa kumfukuzia Muller, licha ya ofa yake kukataliwa. Dau la mwisho aliloweka mezani ni paundi milioni 60.
United wataendelea kujaribu kumsajili Muller na gazeti hilo pia limesema kwamba Van Gaal anamuwinda Gareth Bale.
Tazama ukurasa wa nyuma wa  Sunday Express, huku zikifuatiwa baadhi ya tweets juu ya tetesi hiyo.

 



Comments