Hii ni time lime ya maisha ya kati ya Kleberson na Ronaldo baada ya kusajiliwa na kutambulishwa siku moja ndani ya Manchester united
2003/2004 Ronaldo anasajiliwa na Manchester kwa kiasi cha £ 12.24m kutoka Sporting Lisbon na Kleberson anasajiliwa kwa kiasi cha £6.5m kutoka Atlético Paranaense
2004/2005 Ronaldo anakua mchezaji muhimu wa Manchester united baada ya ku-perfom vizuri kwenye Euro. Kleberson anacheza michezo 6 tu ya ligi.
2005/2006 Ronaldo anasaini mkabata mpya na Manchester United. Kleberson anauzwa kwenda Beskitas kwa £2.5m
2006/2007 Ronaldo anafunga magoli 17 ya EPL na kusaini mkataba mwingine mrefu na Manchester na kutajwa kama PFA Player of year na PFA Young Player of the Year. Kleberson bado anacheza na Beskitas na angalau anashinda Turkish Cup
2007/2008 Ronaldo anashinda EPL na Champions League na kushinda magoli 42 kwenye michuano yote, pia anakua wa pili kwenye Ballon d'Or. Kleberson anajitoa kwenye mkataba wake na Beskitas kutokana na matatizo ya malipo hadi kesi ikabidi ifike FIFA na akasajiliwa kama free agent na Flamengo ya Brazil
2008/2009 Ronaldo anakuwa target ya Real Madrid na kushinda tena EPL, Ballon d'Or na Kleberson angalau ameshinda Seie A na Fmamengo.
2009/2010 Ronaldo anasign na club nyingine kubwa Real Madrid kwa world record fee £80m na kucheza World Cup kama mchezaji mwenye high profile kuliko wote. Wakati huo Kleberson anajiunga na timu ya taifa kwenye world cup na kucheza dakika 9 tu za michuano hiyo
2011/2012 Ronaldo anashinda taji la La Liga kwa mara ya kwanza na anafunga magoli 60 kwenye mechi zote, Kleberson anajiunga na club ya daraja la chini ya ligi kuu inaitwa Atlético Paranaense.
2013/2014 Ronaldo anasaini mkataba mkubwa na Madrid, anashinda Champions League, anashinda Ballon d'Or, kicatu cha dhahabu Ulaya lakini Kleberson anajiunga na Philadelphia Union ya marekani akiwa kama sehemu ya mabadilishano wachezaji.
2014/2015 Ronaldo anafunga magoli 15 kwenye mechi 7 anakuwa mchezaji mwenye kasi kwenye La Liga na kufikia idadi ya magoli 200. Anafunga magoli 61 kwenye mashindano yote na kupiga hat trick 8. Lakini Kleberson anajiunga na ligi ya chini kutoka ligi kuu ya Marekano Major Leagur Soccer
Wawili hawa waliingia pamoja Manchester lakini maisha yao ndani ya hapo yamefunguka kitofauti kupita kiasi. Somo hapa ni kuweka juhudi kila wakati kwenye kazi zetu.
Ronaldo: Scores 200th Real Madrid goal. Champions League top goalscorer.
Kleberson: Goes back to Flamengo. Barely plays. Joins Bahia.
Comments
Post a Comment