DAVID DE GEA : NIPO TAYARI KUKAA LANGONI


DAVID DE GEA : NIPO TAYARI KUKAA LANGONI

DE GEA

Gazeti la daily mail la nchini uingereza, limeripoti kwamba pamoja na kauli alizozungumza kocha wa Manchester United, Louis Van Gaal kwamba David De Gea hayuko sawa kiakili kukaa golini kutokana na sakata lake la kutaka kuhamia Real Madrid, lakini watu wa karibu wa golikipa huyo wamethibitisha ueledi wa mhispania huyo mazoezini na kwamba yuko tayari kukaa langoni.

Kabla ya kuelekea mchezo wa ufunguzi wa ligi dhidi ya Tottenham Hotspur wikend hii, kocha wa Manchester United alimuondoa kikosini David de Gea kwa madai asingekuwa sawa kiakili na kwamba hakuna binadamu anayeweza kumudu hali mbili kwa usawa kwa wakati mmoja.

Lakini inaelezwa kwamba De Gea ameonesha ueledi wa hali ya juu kikosini hapo katika mazoezi na kwamba anajiandaa kucheza katika mchezo wa ijumaa hii dhidi ya Aston Villa katika uwanja wa Villa Park.

Lakini hata hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kocha huyo kuendelea kumtumia golikipa Sergio Romero ambaye ndiye aliyekaa langoni katika mechi dhidi ya Spurs na kuokoa michomo miwili ya hatari. Van Gaal alisema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba huenda De Gea asidake hadi dirisha la usajili litakapofungwa September mwaka huu.

David de Gea amekua akihusishwa na kuhamia Real Madrid ambao hawakubaliani na ada ya pauni 35m Manchester United wanazozihitaji kwa mchezaji huyo aliyebakiza msimu mmoja tu katika mkataba wake.



Comments