COUTINHO AWAPA RAHA LIVERPOOL…


COUTINHO AWAPA RAHA LIVERPOOL…

Aug 9th 2015 - Stoke, UK - STOKE V LIVERPOOL -              Liverpool Courtinho cele PIcture by Ian Hodgson/Daily MailKwa muda mrefu Liverpool ilionekana ingetoka sare ya bila kufungana na klabu ya Stoke City kwenye mchezo wa ligi kuu ya England kwenye uwanja wa Britain Stadium lakini goli la Philippe Coutinho zikiwa zimesalia dakika nne mchezo kumalizika limelipa kisasi cha kipigo cha goli 6-1 ilichopata Liverpool kutoka kwa Stoke City kwenye mechi ya mwisho ya msimu uliopita.

Kikosi cha Brendan Rodgers kimefanikiwa kuondoka na pointi tatu kwenye uwanja wa Britain baada ya kusubiri kwa muda mrefu hatimaye Coutinho akazirejesha pointi tatu kwenye mchezo wao wa ufunguzi ambazo waliziacha hapo kwenye mechi ya mwisho ya kufungia pazia la ligi.

Christian Benteke, Joe Gomez, Nathanie Clyne, James Milner na Firmino walicheza kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha Liverpool wakiwa wachezaji wapya waliosajiliwa kwenye kikosi hicho msimu huu wakati Marco van Ginkel, Glen Johnson na Ibrahim Afellay nao ni wachezaji wapya waliopata nafasi kwenye mchezo wa leo kwa upande wa Stoke City.



Comments