Christian Benteke aliyesajiliwa Liverpool kwa pauni milioni 32.5, ameanza vema kuitumikia timu yake mpya baada ya kufunga bao tamu kwenye mchezo wake wa kwanza kwenye kikosi cha Brenden Rodgers.
Liverpool imeeshinda 2-1 Swindon katika mchezo wake wa mwisho wa maandalizi ya msimu mpya, ambapo Benteke aliyesajiliwa kutoka Aston Villa alifunga bao la kuongoza dakika ya 48.
Jonathan Obika akaisawazishia Swindon dakika 27 kabla ya mchezo kumalizika, lakini Sheyi Ojo akaifungia Liverpool bao la ushindi katika dakika ya 87.
Christian Benteke akishangilia bao lake
Roberto Firmino akimpongeza Benteke
Benteke akifunga kwa shuti kali
Comments
Post a Comment