CHAMBERLAIN AJIBU MAPIGO YA ROY KEANE



CHAMBERLAIN AJIBU MAPIGO YA ROY KEANE
ox
Alex Oxlade-Chamberlain amejibu mapigo kuhusu wanaowakosoa wachezaji wa Arsenal kwa kupiga picha aina ya 'selfies', akidai kuwa wapo makini kuhusu kushindania makombe.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza alifunga goli la pekee katika mchezo wa Ngao ya Jamii uliopigwa Jumapili katika dimba la Wembley ambapo Arsenal waliinyuka Chelsea kwa bao 1-0.
Lakini wakali  wa Emirates wamekosolewa na Roy Keane katika wakati wa maandalizi ya mchezo akisema kwamba wachezaji wa Arsenal wanapenda sana 'selfies' na kuonesha 'six-packs' kuliko kushinda michezo yao.
Hata hivyo,  Oxlade-Chamberlain amekataa madai hayo na kusema kuwa kila mchezaji klabuni hapo anapambana kuhakikisha timu inashinda makombe.
"Ni wakati mwingine huu, au sio? baadhi ya watu wanafanya, wengine wanashindwa," alitanabaisha kuhusu tuhuma za Keane juu yao. "Tuko makini sana kwa kupigania makombe. Mimi binafsi, na pia ninaweza kuwaongelea wenzangu, tumekuwa makini kila mwaka ambao tumekuwa klabuni hapa kushinda ubingwa".
"Unaweza kutazama hayo uwanjani. Watu wengi huwa hawaoni namna gani huwa tunasikitishwa na matokeo mabovu ya timu". 
"Mara zote tumekuwa tukitaka kushinda makombe na miaka iliyopita tumeshinda machache. Na mwaka huu tunataka kufanya vizuri zaidi".


Comments