CATHERINE WA MAPACHA WATATU AMWEKA KWEUPE KHALID CHOKORAA


CATHERINE WA MAPACHA WATATU AMWEKA KWEUPE KHALID CHOKORAA

Mwimbaji pekee wa kike wa Mapacha Watatu, Catherine Chuma ambaye pia amejitosa kwenye muziki wa taarab, amezidi kuweka wazi kuwa yeye na Khalid Chokoraa ni mtu na mume mtarajiwa.

Akiongea katika kipindi cha Shamsham za Pwani cha ITV Jumamosi jioni, mwanadada huyo akasema Chokoraa ni mchumba wake na panapo majaaliwa watafunga ndoa siku za usoni.

Mwimbaji huyo anayetesa na kibao chake cha taarab "Wabaya Watu" akawataka wote wanaopenyeza fitna kwenye uhusiano wake na Chokoraa, waandike maumivu.

"Watu wanahangaika sana, wanasema mimi na Chokoraa hatuwezi kufika mbali, lakini nachukua nafasi hii kuwaambia kuwa nampenda sana Chokoraa na yeye pia ananipenda.

"Hatuna mpango wa kuachana na inshallah panapo majaaliwa yake mola, tutafunga ndoa," alisema Catherine.
 Mahojiano ya Catherine na Hawa Hassan mtangazaji wa Shamsham za Pwani yalivyokuwa yakirekodiwa
Catherine Chuma (kulia) akiwa katika mahojiano na Hawa Hassan (kulia) wa ITV kupitia kipindi cha taarab cha Shamsham za Pwani



Comments