Mkurugenzi            mkuu wa Manchester United, Ed Woodward yupo mjini Barcelona,            Hispania kujaribu kufanya mazungumzo ya kumsajili Pedro kwa            paundi milioni 22.
        Woodward            alikwea pipa jana kwenda  Catalunya kushuhudia mechi ya            marudiano ya Spanish Super Cup kati ya Barcelona na Athletic            Bilbao iliyopigwa uwanja wa Camp Nou.
        Inafahamika            kwamba bosi huyo wa Old Trafford anatarajia kufikia hatua            nzuri ya kukamilisha dili hilo, huku Chelsea nao wakihusishwa            kuvutiwa na nyota huyo.
        
Comments
Post a Comment