BAYERN MUNICH YAIKATA MAINI MANCHESTER UNITED KUHUSU SAINI YA THOMAS MULLER



BAYERN MUNICH YAIKATA MAINI MANCHESTER UNITED KUHUSU SAINI YA THOMAS MULLER

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich Matthias Sammer amsema hakuna uwezekano wa mshambuliaji wao Thomas Muller kujiunga na Manchester United.
Muller mwenye umri wa miaka 25 amekuwa akihusishwa na usajili wa bei mbaya wa kwenda Manchester United kiangazi hiki ambapo Mashetani Wekundu wanatajwa kuandaa ofa ya pauni milioni 60.
Huku nahodha wao Wayne Rooney akiwa butu, mashabaki wa United wanamtaka kocha Louis van Gaal kusajili mshambuliaji mwingine.
Lakini Sammer ambaye katika enzi zake za kusakata kabumbu alizitumikia Inter Milan and Borussia Dortmund, amesema hakuna mchezaji mwingine akatakayeondoka Bayern Munich kiangazi hiki.
"Tutahitaji kila mchezaji," alisema Sammer katika maongezi yake na waandishi wa habari wa Ujerumani na kuongeza: "Nadhani kitu kama hicho hakiwezi kutokea."





Comments