BAADA YA KIPA WA WEST HAM KULIMWA KADI NYEKUNDU, MCHEZAJI HUYU AKAVAA GLOVES NA KUKAA GOLINI

BAADA YA KIPA WA WEST HAM KULIMWA KADI NYEKUNDU, MCHEZAJI HUYU AKAVAA GLOVES NA KUKAA GOLINI
Jenkinson akielekea langoni kuchukua mikoba ya Andrian

Jenkinson akielekea langoni kuchukua mikoba ya Andrian

Carl Jenkinson, ilimlazimu kucheza kama kipa jana katika mchezo kati ya West Ham dhidi ya Leicester ambapo West Ham walipoteza mchezo huo kwa mabao 2-0, mchezo uliopigwa katika dimba la Upton Park, maskani kwa West Ham.

Wagonga nyundo hao walikuwa wameshamaliza idadi ya wachezaji wao wanaotakiwa kufanyiwa mabadiliko, mbaya zaidi ni pale kipa wao Adrian alipopewa kadi nyekundu na kumlazimu kutoka nje huku wakiwa hawaruhusiwi tena kufanya mabadiliko.

Kipa wa West Ham Andrian akizawadiwa kadi nyekundu

Kipa wa West Ham Andrian akizawadiwa kadi nyekundu

Hapo ndipo mchezaji wa Arsenal anaecheza kwa mkopo katika klabu hiyo Jenkinson alipopelekwa langoni ili kuziba nafasi ya Andrian na kufanya vema kabisa akiwa langoni hapo.

"Nilihisi kadi ile nyekundu ilikuwa kidogo ya kikatili, sawa alinyoosha mguu juu lakini ilikuwa ni kwa bahati mbaya", alisema mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uingereza U-21 baada ya mchezo.

Mlinda mlango mpya: Jenkinson akiondoa hatari lango              akiwa na jezi mpya kama golikipa

Mlinda mlango mpya: Jenkinson akiondoa hatari lango akiwa na jezi mpya kama golikipa

"Ilinibidi nikakae mimi golini lakini nashukuru sikuwa na kazi kubwa sana ya kufanya maana sikupata rapsha nyingi".

Jenkinson 3

Comments