Arsenal wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani, wamelazimishwa sare ya 0-0 na Liverpool katika mchezo mgumu wa Premier League.
Liverpool walitawala vizuri katika dakika 45 za kwanza lakini kipa wa Arsenal Petr Cech aliyeng'ara vilivyo akawa shujaa kwa kuondoa michomo ya hatari kutoka kwa Christian Benteke na Philippe Coutinho.
Hata hivyo ni Arsenal watakaoumizwa zaidi na sare hii baada ya kiungo Aaron Ramsey kufunga bao safi dakika ya 9 lakini kwa mshangao wa wengi mwamuzi Michael Oliver akalikataa kwa madai ya kuwa mfungaji alikuwa ameotea.
Liverpool bado hajaifungwa hata goli moja tangu msimu huu ulipoanza baada ya kushinda mechi zake mbili za mwanzo dhidi ya Stoke City na Bournemouth.
ARSENAL (4-2-3-1): Cech; Bellerin, Chambers, Gabriel, Monreal; Coquelin (Oxlade-Chamberlain 82mins), Ramsey; Ozil, Cazorla, Sanchez; Giroud (Walcott 73)
LIVERPOOL (4-3-3): Mignolet; Clyne, Lovren, Skrtel, Gomez; Can, Milner, Lucas (Rossiter 76); Coutinho (Moreno 88), Firmino (Ibe 63), Benteke.
Petr Cech akiruka na kupangua kwa mkono wa kushoto shuti la karibu la Benteke
Comments
Post a Comment