ARSENAL IMJENGWA VIZURI SANA, UKIITOA CHELSEA


ARSENAL IMJENGWA VIZURI SANA, UKIITOA CHELSEA

Arsenal 22

Na Joel Chuku

Arsenal ni timu ambayo inapewa nafasi kubwa ya kufanya viuri kwenye ligi kuu England msimu huu kutokana na kiwango ilichokionesha kuanzi kwenye mechi za pre-season mpaka mchezo wa kuwania ngao ya jamii ilipocheza na Chelsea na kuifunga kwa goli 1-0 hatimaye kutwaa ngago ya jamii.

Ni ambayo imeonekana kujegwa na kusukwa upya pia ukiongeza ujio wa golikipa Petr Cech aliyesajiliwa kutoka klabu ya Chelsea na kuonesha uwezo mkubwa tangu aanze kukaa kwenye lngo la Arsenal.

Labda  kidogo na Man City japo wanapitia matatizo kidogo ila matatizo yao ni ya Pellegrin kujitakia, anaweza kuyafuta haraka matatizo hayo ila ni timu nzuri pia Chelsea wamekaa juu ya Arsenal kwakua wao walishadevelop kikosi chao muda mrefu uliopita na hiki kikosi chao kipya kilishatoa matunda msimu uliopitakwahiyo automatically wapo juu kuliko timu yeyote pale England..

Msimu wa 2013/2014 Arsenal iliongoza league kwa siku128 ikiwa kipindi kirefu kuliko vyote kwa msimu ule na majeruhi ndio yaliharibu msimu ule kwa Arsenal. Ila mnajua nini kilitokea majira ya kiangazi ya 2014, Alikuja fitness coach mpya na hata statistics za majeruhi zilipungua kutoka 2013/2014 zikawa zimepungua kwa asilimia kubwa msimu wa 2014/2015.

Kitu kilichofanya Arsenal kuanza ovyo msimu uliopita wa 2014/2015 ni kwakua tulikua na muhimu wengi waliokosa pre-season kuliko walioenda pre-season hii ikawa shida kuifanya timu iwe na moto mapema na wachezaji kuumia na walikosa maadaliz mauzri.

Mzunguko wa pili wa kuanzia January baada ya timu kuchanganya kwenye ligi kwa hesabu za haraka haraka ilipoteza game mbili tu halafu hata draw zenyewe zilikua chache sana, ilitoka nafasi za nje ya top four tukamaliza namba tatu halafu leo hii utasemaje team ya Arsenal bado sana? Arsenal haihitaji mbadala wa Cazorla.

Kuna namba nane bora sana mwingine anacheza winger (Ramsey) kwasababu ya huyo cazorla, na kama Cazorla akiumia, Ramsey anarudi kwenye nafasi yake nafasi iliofanya mashabiki wa timu nyingine wamuelewe kwenye msimu wa 2013/2014.

Chaguo la tatu kwa kucheza namba nane pale Arsenal ni Jack Wilshere sasa club gani pale England namba nane wake chaguo la tatu yuposawa na Wilshere wa Arsenal bwana mdogo anae kimbiza kwenye timu ya taifa ya England.

Arsenal inahitaji defensive midfielder (kiungo mkabaji) mzuri zaidi mwingine hapo ni kweli hamna ubishi ila kuhusu magoli, Arsenal ndio timu yenye mlinganyo mzuri wamagoli kuliko timu yeyote pale Premier League.

Hivyo ndivyo ilivyo. Olivier Giroud hayupo pale kucheza kama Diego Costa au Kun Aguero kwa maana asimame kama one goal machine.

Giroud ni team player ndio kitu Wenger anapenda na ndio kitu kilichofanya Arsenal ifunge magoli 106 msimu uliopita ikiwa timu pekee England kufanya hivyo. Ilifanya hivyo huku Giroud mwenyewe akiwa majeruhi miezi mitatu, Ozil miezi mitatu, Walcott alianza kucheza January kwahiyo, tuseme miezi sita na hawa wote hua wanachangia sana magoli ndani ya timu.

Kitu kilichopo hapa ni kwamba, Arsenal ina inawania ubingwa na inanaweza kuupata kwa hivi walivyo kwasasa na kama Arsenal inachukua mtu kama Benzema na kiungo mkabaji mzuri ni moja kwa moja inanakua favorite kubebataji la ligi kuu England, ila kocha atawasajili pale watakapokua wana na nafasi ya kucheza kwa maana watakapo julikana wazi ni vipi watasaidia timu na style gani watacheza.

Kuna baadhi ya Guners wanalia wanataka striker mpya, hiki ni kitu kibaya sana, mnaweza kuletewa Lionel Messi au Ronaldo mkajikuta mna mnaharibu mfumo mzima wa timu ili kuweza kuwa kuwapa nafasi hao wachezaji, je mpo tayari kuharibu kazi uliyoianza misimu kibao nyuma?

Louis van Gaal mwenyewe alianza kuinoa timu yake msimu uliopita kaona isiwe tabu kamuachia Di Maria aende zake kwakua alikua hakai sawa kwenye mfumo wake japo alimsajili yeye mwenyewe na kwa mapenzi yake kila kocha anaangalia kipi bora kwa timu yake kuliko ubora wa mchezaji mmojammoja.

Wenger ndiye alimnoa Henry anajua ni ubora upi Henry anao tofauti na Giroud anajua Giroud anazingua wapi solution yake itakuja muda muafaka wa kufanya hivyo ukifika.

Mashabiki wanapenda sana kujirundikia wachezaji wapya bora kwakua tu ni mashabiki ila elimu ya kuinoa team hawana.

Msimuu huu wa 2015/2016 Arsenal inaweza kuchukua taji kama tikikaza ila sio kwa kikosi chenye nguvu kama kitakachokuwepo mwakani kwakua nahisi kwa sasa haiwezi kusajili striker na kiungo mkabaji kwa mpigo kwa dirisha hili la usajili.

Arsenal hii imeanza kupikwa tangu 2012 alivyouzwa Van Persie na kuja akina Cazorla msimu ule hii team imekua kitimu na kila msimu wanaiboresha na hiyo ndio njia pekee ya kushinda taji la ligi kuu, huwez kushinda taji la ligi kwa kukiandaa kikosi chako kwa miezi miwili ya mapumziko ya ligi au kwa msimu mmoja tu.

Arsene Wenger alipoona hamna sababu ya kumrudisha Fabregas kikosini ilikua ni statement tosha ni jinsi gani yupo makini kwa kuisuka hii timu.

Kila mtu anajua makali ya Fabregas yalivyo hilo halina ubishi ila kama angerudi ni wazi angekuja kuharibu system nzima ya timu kwakua lazima ungeleta mfumo mpya wa kumfanya Fabregas acheze kwenye kikosi.

Timu bora sio kurundikarundo la wachezaji wa gharama, timu bora ni kuifanya icheze vizuri kwa kiwango cha juu na kitimu.

Kikosi cha Asenal kilichoongoza ligi hadi April kwenye msimu wa 2007/2008 na ikaja kuishia nusu fainali ya Champions league 2009 ile timu ilikua ni timu bora bila hata gharama kubwa, ila tu kipindi kile ilikuwa inashindwa kukaa na wachezaji bora kwa shida za kiuchumi ililazimika kuuza na kuijenga upya ila timu ile ingekua haina shida za kiuchumi na ingeendelea kukaa pamoja ingefika mbali sana wakati hata haikutumia zaidi ya £15 kununua mchezaji.

Arsenal ya sasa imenolewa muda sasa na kila siku inaongezewa vitu vipya tena kwa uangalifu wa hali ya juu ili isiharibiwe system nzima haijibebei tu wachezaji.

Swala la kuuza, kununua wachezaji na kuwawekakwenye system hasa kwenye ligi yenye ushindan wa timu nyingi kama England sio jambo rahisi hata kidogo.

Team hua inasukwa, wachezaji wa gharama hua wananunuliwa, ukiwa na wachezaji wa gharama sio tiketi ya ya kuchukua ubingwa..

Uzuri wa wachezaji wa world class labda hautakaa miaka mingi sana kusuka timu ila ni lazima uisuke kwanza.



Comments