Mabingwa wa ngao ya jamii timu ya Arsenal imekubali kipigo cha goli 2-0 kutoka kwa West Ham United kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka England mchezo uliomalizika muda mchache kwenye uwanja wa nyumbani wa Arsenal Emirates jijini London na kupoteza pointi tatu za kwanza kwenye mechi yao ya kwanza msimu huu.
Petr Cech aliyesajiliwa majira haya ya kiangazi akitokea Chelsea aliukosa mpira alipotokea kwenda kujaribu kuokoa mpira wa adhabu ndogo na kumruhusu Kouyate kupiga kichwa kwenye lango ambalo lilikiuwa halina mtu dakika mbili kabla ya mapumziko.
Zarate ambaye alikuwa na kiwango bora msimu uliopita akiwa QPR kwa mkopo alifanya mambo yaendelee kuwa magumu kwa upande wa Arsenal baada ya kufunga goli la pili kwa shuti dogo lililomshinda mlinda mlango Petr Cech na kutinga wavuni ikiwa ni dakika ya 57 ya mchezo.
Mchezo mwingine uliomalizia ulikuwa ni kati ya Newcastle United dhidi ya Southampton uliomalizika kwa timu izo kutoka sare ya kufungana bao 2-2 kwenye mwendelezo wa ligi kuu nchini England maarufu kama EPL.
Graziano Pelle alianza kuifungia Southampton goli la kuongoza baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi ya Cedric Soares kabla ya Papiss Cisse hajaisawazishia Newcastle kabla ya kwenda mapumziko.
Georginio Wijnaldum aliyesajiliwa na Newcastle akitokea PSV Einhoven aliifungia Newcastle goli la pili akiunganisha krosi iliyopigwa na Gabriel Obertan lakini Southsampton walisawazisha goli hilo kupitia kwa Shane Long na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa timu hizo kwenda sare ya kufungana goli 2-2.
Comments
Post a Comment