UNAJUA WACHEZAJI WA PARAGUAY WAMEAHIDIWA NINI KUELEKEA MCHEZO WA NUSU FAINALI DHIDI YA ARGENTINA? WAKISHINDA WATAPATA ZAWADI HIII…



UNAJUA WACHEZAJI WA PARAGUAY WAMEAHIDIWA NINI KUELEKEA MCHEZO WA NUSU FAINALI DHIDI YA ARGENTINA? WAKISHINDA WATAPATA ZAWADI HIII…

argentina vs paraguayWachezaji wa mpira wa miguu wamekuwa wakiahidiwa zawadi mbalimbali kama vile pesa, nyumba za kifahari pamoja na likizo au mapumziko, lakini gairi aina ya pick-up? Tena sio moja, ni tatu…hicho ndicho walichoahidiwa wachezaji wa kikosi cha Paraguay endapo watafanikiwa kuifunga Argenina kwenye mchezo wa nusu fainali ya Copa America utakaochezwa usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano.

"Nimewaahidi chochote wachezaji? Waulize wachezaji, wameshashinda zawadi mbili", amesema kocha wa Paraguay Ramon Diaz.

Mshambuliaji Edgar Benitez aliongeza: "Tayari tumeshashinda pick-up mbili kutoka kwake na tunaenda kwenye ya tatu".

Wakati huohuo, Diaz amesema anataka kulipa kisasi kwa kushindwa kufuzu kucheza kombe la dunia la mwaka 2014 kufuatia kufungwa na Argentina kwenye mchezo wa mwisho wa kufuzu kwa kichapo cha goli 5-2 mwaka 2013.

"Naamini timu hii ina kiu ya kulipa kisasi, ndiomaana tumefikia hatua hii", amesema.



Comments