RAHEEM STERLING AFUZU VIPIMO VYA AFYA MANCHESTER CITY


RAHEEM STERLING AFUZU VIPIMO VYA AFYA MANCHESTER CITY
Raheem Sterling amepiga hatua nyingine kuelekea usajili wake wa pauni milioni 49 kwenda Manchester City baada ya kufuzu vipimo vya afya Jumanne hii.

Winga huyo wa Liverpool sasa anaelekea kutimiza ndoto yake ya kuondoka Anified baada ya msuguano wa muda mrefu juu ya hatma yake.

Jumapili iliyopita vilabu hivyo viwili vikafikia muafaka wa kufanya biashara na sasa baada ya Raheem kufuzu vipimo vya afya, Manuel Pellegrini anategemewa kumsajili mchezaji huyo chaguo lake kuu kiangazi hiki.

Raheem Sterling mambo safi, safari ya Man City imeiva
Sterling leaves the hospital on Tuesday afternoon      Sterling verge of completing Manchester City                  switch
Sterling akitoka hospitalini kufanya vipimo vya afya
Sterling signs a football for a fan as he is stopped                outside the hospital following his medical
Sterling akiweka saini kwenye mpira wa kibabu shabiki wa Manchester City nje ya hospitali alipokwenda kufanya vipimo vya afya



Comments