Raheem Sterling            amekunjua makucha yake na kuwaambia Liverpool kuwa hataki            kuandamana na timu hiyo katika ziara yao ya mashariki ya            mbali.
        Licha ya winga            huyo kushiriki mazoezi ya kujindaa na msimu mpya, lakini            anataka kubaki England ili ajipange na mpango wake wa kutaka            kuihama Liverpool.
        Raheem ameonyesha            wazi kuwa hana nia ya kuendelea kuitumikia Liverpool na sasa            anaingia kwenye hatua ambayo inaonekana kama ni mwelekeo wa            kulazimisha kuuzwa.
        Manchester City            bado haijapeleka ofa ya tatu huku mbili zikiwa zimepigwa chini            na Liverpool ambayo inataka ilipwe pauni milioni 50 kwa kinda            huyo wa miaka 20.
        Andre Wisdom na Raheem              Sterling (mbele) wakiwa mazoezini siku ya Jumatatu
        Sterling ameripoti              Melwood Training Ground  Julai 6 licha ya mipango yake ya              kutaka kutimka Liverpool
          Sterling                akiwasili mazoezini na Mercedes yake nyeupe
          Liverpool                imeshakataa ofa mbili za Manchester City £35million na                 £40million 
          
Comments
Post a Comment