Mesut Ozil amekabidhiwa jukumu la kucheza kama namba 10 likiwa ni jukumu lake jipya kwa msimu ujao.
Hiyo ni hatua ya kocha wa Arsenal Arsene Wenger ya kutafuta njia sahihi ya kumfanya mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa pauni milioni 24 aonyeshe uwezo wake uliotarajiwa na wengi.
Ozil anayeshikilia rekodi ya usajili wa bei mbaya kwa Arsenal alikuwa akichezeshwa katika mfumo wa viungo washambuliaji watatu ambao ulishindwa kumweka katika ubora wake.
Lakini sasa atacheza nyuma ya mshambuliaji namba 9 huku Alexis Sanchez akihamishiwa kucheza kama winga.
Mesut Ozil (katikati) sasa atacheza kama namba 10
Ozil ameshindwa kung'ara Emirates katika nafasi ya kiungo
Comments
Post a Comment