Uefa wamedhibitisha kuwa fainali ya klabu bingwa Ulaya mwaka 2017 itafanyika kwenye uwanja wa Millennium Stadium uliopo uliopo Cardiff, Wales.
Mchezo huo utapigwa Machi 3, 2017 wakati fainali ya klabu bingwa Ulaya kwa upande wa wanawake itapigwa siku mbili kabla kwenye dimba la Cardiff City Stadium.
Uwanja huo wa Millennium Stadium unauwezo wa kubeba mashabiki 74,000 waliokaa ulishawahi kuchezewa mchezo wa fainali ya FA Cup, mchezo wa ngao ya jamii (Community Shield) na michezo ya mtoano kuwania kucheza ligi kuu tangu mwaka 2001 hadi 2006.
Michezo ya mpira wa miguu ya Olympic mwaka 2012 pia ilipigwa kwenye uwanja huo.
Dimba hilo ambalo lipo katikati ya jiji la Cardiff, Wales litatumika pia kwa ajili ya mechi za fainali za kombe la dunia la mchezo wa Rugby mwaka huu.
Mshambuliaji wa Real Madrid ambaye ni mzaliwa wa jijini Cardiff Gareth Bale amesema, "itakuwa ni furaha kubwa kujumuika mbele ya mashabiki lukuki kwenye uwanja wa kipekee mwaka 2017"
Chama cha mpira wa miguu nchini Wales (FAW) ndio waliibuka vinara wa mbio za kuandaa moja ya fainali kubwa za Uefa kwa kushirikiana na Chama cha mchezo wa Rugby ambao ndio wamiliki wa uwanja wa Millennium Stadium.
Mkurugenzi mkuu wa FAW Jonathan Ford aliikaribisha bodi inayo ratibu masuala ya soka la Ulaya kwa ajili ya kutangaza tukio hilo.
"Tunamini kwamba kwa kuanza na fainali zote za vilabu bingwa Ulaya mwaka 2017 kwa wanaume na wanawake, zitaleta changamoto chanya kwenye soka la Wales", alisema Ford.
"Leo nawashukuru wote walioshiriki kuisaidia FAW kukamilisha tukio hili baada ya kazi nzuri na nzito ya miaka miwili".
Rais wa FAW Trefor Lloyd Hughes amesema: "Soka la Wales linapanda juu na tunatazama mbele na kushirikiana na Uefa na wadau wetu wote kwa miaka miwili ijayo ya fainali za kukumbukwa".
Naye mtendaji mkuu wa WRU Roger Lewis amesema: "Millennium Stadium ni moja kati ya viwanja bora vya michezo Ulaya na ninaimani itakuwa ni sehem nzuri kwa ajili ya fainali ya Uefa".
Mji huo mkuu wa Wales unahistoria ya kuandaa michuano ya michezo mingi mikubwa ikiwa ni pamoja na fainali za kombe la dunia za mchezo wa Rugby mwaka 1993.
Cardiff City Stadium ulitumika kwenye mchezo wa fainali ya Super Cup mwaka 2014 ambapo Real Madrid ilishinda kwa kuifunga timu ya Sevilla.
Comments
Post a Comment