Sentahafu wa            Borussia Dortmund Mats Hummels ameweka wazi kuwa hana mpango            wa kutimka klabuni hapo msimu huu.
        Hata hivyo, beki            huyo mwenye umri wa miaka 26, mshindi wa kombe la dunia,            ameshindwa kuihakikiashia timu hiyo iwapo atakuwa na maisha            marefu kwao baada ya kusema atakuwepo hapo angalau kwa mwaka            mmoja zaidi.
        Habari hizo za            Hammels zinakuwa ni pigo kubwa kwa Manchester United ambao            tangu mwaka jana wamekuwa wakihangaika kupata saini yake.
        Hemmels mwenyewe            anasema ni jambo la kuvutia kuwindwa na timu kama Manchester            United lakini kwa sasa bado anahitaji kuendelea kukaa            Ujerumani.
        Huku washkaji            zake  Mario Gotze na Robert Lewandowski wakiwa            wameshatimka Borussia Dortmund katika vipindi tofauti, Hammels            anaona kwa upande wake si jambo sahihi kuitosa klabu hiyo            msimu huu.
        Mats Hummels wa                Borussia Dortmund akiwasabahi washabiki wa timu hiyo huko                Singapore siku ya Jumatano
        Hummels akifurahi                kwenye mkutano wa waandishi wa habari kwenye hotel ya                Fullerton huko Singapore
        Hummels akiwa              mazoezini na wachezaji wenzake huko Mashariki ya mbali
        
Comments
Post a Comment