MARCOS ROJO anaamini Angel Di Maria ndiye mchezaji mwenye kipaji zaidi katika Manchester United na anaamini winga huyo atarejea kwenye uhalisia wake msimu ujao.
Di Maria alijunga na Manchester United kiangazi kilichopita akitokea Real Madrid kwa pauni milioni 59.7 ambayo ilikuwa rekodi mpya ya usajili Uingereza, lakini kinyume na matarajio ya wengi, akashindwa kung'ara Old Trafford.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 alifunga magoli matatu katika mechi zake tano za mwanzo lakini hali ikageuka baadae na akakumbwa na ukame wa magoli huku akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara.
Lakini mchezaji - Marcos Rojo - anayekipiga na Di Maria katika timu ya taifa ya Argentina na Manchester United, anasema anaamini makali ya mshambuliaji huyo yatarejea sehemu yake msimu ujao.
Comments
Post a Comment