Kocha huyo raia wa Chile                aliponea chupuchu kutimuliwa kiangazi hiki licha ya                kumaliza bila taji lolote.
            Lakini inaeleweka kuwa                mwenyekiti wa Manchester City Khaldoon Al-Mubarak amepania kumchukua                kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola miezi 12 ijayo.
            Kwa hali hiyo, Pellegrini                anaweza akajikuta anaitumikia City kwa mwaka wa mwisho kwa                vile klabu hiyo haijaonyesha dhamira ya kurefusha mkataba                wake. 
                        Khaldoon Al-Mubarak amepania kufanya                  usajili wa kishindo kiangazi hiki, hali inayompa imani Pellegrini kuwa anaweza kuwa na                  kikosi kizuri kitakachookoa kibarua chake.
              Pellegrini, 61, anaamini anaweza                  akashinda taji la Premier League pamoja na Champions                  League na hivyo kuwa kishawishi cha kupewa mkataba mpya.
            
Comments
Post a Comment