Manchester United            inakaribia kumsajili beki wa kulia wa Kitaliano Matteo Darmian baada ya majadiliano na            klabu yake ya Torino kufikia hatua nzuri. 
        United imekuwa            ikisaka kwa udi na uvumba beki wa kulia baada ya kocha wake  Louis van Gaal kuamua            kuwa Rafael si mtu sahihi.
        Manchester United            wanaaminika kuwa watafanikiwa kumsajili mchezaji huyo mwenye            umri wa miaka 25 kwa ada inayokisiwa kufikia pauni milioni 11.
        Matteo Darmian                (kulia) anakaribia kutua United
        Kwa  muda Manchester                United imekuwa ikisaka beki wa kulia na sasa beki huyu wa                kimataifa wa Italia anaelekea kukata kiu yao
        
Comments
Post a Comment