MANCHESTER UNITED YAAMBIWA NA SOUTHAMPTON RUKSA KUMSAJILI MORGAN SCHNEIDERLIN LAKINI SI KWA PESA YA 'KITOTO'
Southampton imesema            haitamzuia Morgan Schneiderlin  kujiunga na Manchester United lakini            kocha wake Ronald Koeman            ametahadharisha kuwa klabu hiyo ya Old Trafford lazima itoe            mshiko mnene.
        United ilipeleka            ofa ya pauni milioni 20 kwaajili ya Schneiderlin lakini wameambiwa wakajipange upya na            wajiongeze hadi kitu kinachokaribia pauni milioni 30 kama            kweli wahahitaji huduma ya kiungo huyo wa kimataifa wa            Ufaransa.
        "Kila mchezaji ana            thamni yake na tuna uzoefu wa kutosha wa kuuza wachezaji,"            anaeleza Koeman. "Kama kuna dili la kumtaka Morgan Schneiderlin ni sawa ila lazima iwe            kwa pesa tunayotaka."
        "Ni mchezaji wetu            muhimu, ni mchezaji wa kimataifa. Lakini hilo sidhani kama ni            tatizo kwa Manchester United."
         Manchester United              wanatakiwa kuongeza mshiko ili kumpata Morgan Schneiderlin
        United ilidhani ofa yao              ya pauni milioni 20 ingetoshasha kumnasa kiungo huyu wa              kimataifa wa Ufaransa
        Koeman dau la milioni              20 ni utani, halilingani na uwezo wa mchezaji wao
        
Comments
Post a Comment