Klabu            ya Mnchester United inakaribia kukamilisha dili la kumsajili            beki wa kulia Matteo Darmian baada ya majadiliano kati ya            United na klabu ya Torino ya Italia kufikia hatua nzuri.
United wanahitaji mchezaji ambaye anaweza akacheza kama mlinzi wa kulia baada ya kocha wa kikosi hicho Louis van Gaal kusema kwamba, mbrazil Rafae ameshindwa kuimudu nafasi hiyo.
Ieleweke kwamba, Man United imekuwa kwenye mazungumzo na Darmian, 25, na wanamatumaini ya kufikia makubaliano ya kumsajili nyota huyo kwa kiasi cha pauni milioni 11.
Darmian ni mchezaji wa kimataifa wa Italia ambaye ameshaitumikia timu yake ya taifa kwa michezo 13 na michezo sita akicheza muda wote (full time), Van Gaal anaamini mchezaji huyo atamsaidia kwenye nafasi ya ulinzi wa kulia.
Pia            Van Gaal anatarajia kumuachia Rafael aondoke kabla ya kuanza            kwa msimu mpya lakini atasikiliza ofa pia juu ya mlinzi wa            kati John Evans ambaye mpaka sasa bado hajapewa mkataba mpya.
Comments
Post a Comment