Liverpool imeanza kujiandaa na maisha bila Raheem Sterling baada ya kupaa kuelekea kwenye ziara yao ya Mashariki ya Mbali bila winga huyo anayekaribia kutua Manchester City.
Raheem anakwenda City kwa pauni milioni 45 ambapo maofisa wa klabu hiyo wameidokeza Daily Mail la Uingereza kuwa usajili huo unakaribia kukamilika.
Brendan Rodgers akiwasili Manchester Airport wakati kikosi chake cha Liverpool kikijiandaa kupaa kwenda Asia kwa maadalizi ya msimu mpya
Raheem Sterling hajasafiri na Liverpool ili kukamilisha usajili wake na Manchester City
Nathaniel Clyne (katikati) na Danny Ings (kulia) ambao wote wamejiunga na Liverpool kiangazi hiki na wapaa kuelekea Mashariki ya Mbali
Mchezaji mwingine ambaye hajaondoka na Liverpool ni mshambuliaji Mario Balotelli.
Inaaminika mchezaji huyo mtukutu wa Italia naye siku zake za kuishi Liverpool zinahesabika.
Comments
Post a Comment