Joan Laorta ambaye anawania nafasi ya urais kunako klabu ya FC Barcelona amesema anatarajia kumsajili kiungo wa Juventus Paul Pogba kama atachaguliwa kuwa rais wa klabu hiyo mwezi ujao.
Pogba, 22, amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu nyingi za Ulaya ikiwemo Real Madrid, Paris Saint- Germain na Manchester City licha ya kwamba ada yake ya uhamisho kuwa ni Euro milioni 100.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa akizungumzwa sana huku akihusishwa na muwania urais wa Camp Nou Laporta pamoja na mtendaji mkuu wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu wote kwa pamoja wamesisitiza kuwa watahakikisha wanainasa saini ya Pogba.
Gazeti la michezo la Catalan la wiki hii limeandika kwamba, wawakilishi wa klabu hiyo wanajipanga kukutna na Juve kujadili uhamisho wa mchezaji huyo licha ya ukweli kwamba, Barca haitakuwa na rais wala bodi hadi baada ya uchaguzi wa Julai 18 na wakati huo wakiwa wamefungiwa kusajili wachezaji wapya hadi Januari 2016.
Laporta anafahamu fika hakutakuwa hakutakuwa na tatizo kuhusu kumsajili mchezaji huyo kwasababu wanafahamiana vizuri na wakala wa Pogba wakati akimsajili moja kati ya wateja wa wakala huyo Zlatan Ibrahimovich wakati alipokuwa rais wa Barcelona.
Wakati akihojiwa kwenye kipindi cha redio "El Partido de las 12" amesema: "mtu pekee atakaemrahisishia kumnasa Pogba ni Mino Raiola. "Ni kweli kwamba nina uhusiano mzuri sana na Raiola na ninaamini kama nikiwa rais, Pogba atacheza Barcelona".
"Nafikiri bodi inakutana na Juve, lakini mtu wa kuzungumza nae ni Raiola, yeye ndie mwenye funguo".
"Pogba ana ubora wa hali ya juu, na anaendana na aina ya soka la Barca. Ingawa ana gharimu kiasi kikubwa cha pesa lakini ni kielelezo cha mchezaji kama Neymar, Suarez, na Ronaldo ambao pia wanagharimu pesa nyingi".
Taarifa zinasema kwamba, Pogba, Koke, Isco, na Di Maria ni wachezaji ambao wanahusishwa kusajiliwa na Barcelona lakini Laporta amedai kuwa, kocha wa klabu hiyo amekuwa akihitaji kiungo.
Comments
Post a Comment