Timu ya Taifa ya            Argentina imetinga kwa kishindo hatua ya fainali ya Copa            America baada ya kuitandika Paraguay kipigo cha mbwa mwizi cha            magoi 6-1 katika mechi ya nusu fainali iliyopigwa usiku wa            kuamkia leo.
        Mabao ya Argentina            yamefungwa na Marcos Rojo (15), Javier Pastore (27), Angel Di            Maria (47, 53), Sergio Aguero (80) na Gonzalo Higuain (83),            huku goli la kufutia machozi kwa Paraguay likifungwa na Lucas            Barrios (43).
        Kama kocha wa Manchester            United, Louis van Gaal anataka kupata kiwango cha Di Maria,            labda amsajili Lionel Messi na kama anashindwa kufanya hivyo,            basi amnase Javier Pastore.
        Hawa watu walimfanya Di            Maria apige soka la kiwango cha juu kutokana na pasi maridhawa            walizokuwa wanammegea.
        Messi alionesha kiwango            kizuri na kujaribu kufunga mara kadhaa, lakini bahati haikuwa            upande wake.
        
Comments
Post a Comment