BEKI MATTEO DARMIAN AKUBABALI KUJIUNGA NA MANCHESTER UNITED ...ada ya pauni milioni 12 na mkataba wa miaka minne
Beki Matteo Darmian amethibitisha kuwa anajiunga na Manchester United baada ya kukubali dili la mkataba wa miaka minne.
United imekubali kuilipa Torino pauni milioni 12.7 lakini zitafika hadi 14.4 kutegemea na namna atakavyong'ara Old Trafford.
AC Milan, klabu ya zamani ya Darmian nayo itapokea pauni 287,000 kama asilimia tano ya mauzo hayo hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa mkataba waliouweka wakati wanamuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.
Darmian ameichezea Italia mechi 13 na kimo chake kinachokaribia futi 6 kitamsaidia Van Gaal kutatua moja ya matatizo yaliyomkabili msimu uliopita.
Van Gaal alitaja sula la vimo vya wachezaji kama moja ya vitu vinavyohitaji kufanyiwa uwiano kwenye kikosi chake.
Usajili rasmi wa Darmian unatarajiwa kutangazwa masaa 24 yajayo.
Matteo Darmian akiichezea Italia katika mechi za kufuzu Euro 2016 dhidi ya Bulgaria mwezi Machi
Darmian (kulia) akifunga dhidi Juventus mwezi April
Comments
Post a Comment