Mario Balotelli amewataka            mashabiki wa Liverpool kumsapoti Raheem Sterling baada ya            kuondoka klabuni hapo kujiunga na Manchester City.
        Sterling leo amecheza            mechi yake ya kwanza katika kikosi cha Man City chini ya            Manuel Pellegrini.
        Katika mechi hiyo ya            kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya, Sterling amefunga goli            katika sare ya 2-2 ndani ya dakika za kawaida, kabla ya Man            City kushinda kwa penalti 5-4.
        Muda mfupi baada ya            mechi, Super Mario ame-tweet kumpongeza Sterling kwa kuanza            vizuri.
        Mashabiki wengi wa            Liverpool  wanaona Sterling ni msaliti kwasababu ya            kulazimisha kuondoka Anfield.
        Soma Tweets za Mario hapo            chini akiwajibu mashabiki wa Liverpool wenye hasira:
                                
Comments
Post a Comment