ASAMOAH GYAN KULIPWA MSHAHARA WA ZAIDI YA £163,000 KWA WIKI



ASAMOAH GYAN KULIPWA MSHAHARA WA ZAIDI YA £163,000 KWA WIKI

a1
Mpira ni pesa, hakuna fujo wala figisufigisu. Mchezaji wa Ghana ambae aliwai kucheza kwenye Sunderland kwenye ligi ya uingereza anaendelea kupiga pesa nyingi baada ya kuhama kwenye club za ulaya.

Hivi sasa anahama kutoka club ya Al Ain ambayo makazi yake yapo Abu Dhabi na kujiunga na club ya Shanghai SIPG. Asamoah ameonekana akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Shanghai akienda kwenye kazi moja tu ambayo ni kusaini mkataba na club hiyo ambayo inafundishwa na kocha Sven-Goran Eriksson.

Asamoh anatarajia kulipwa mshahara mkubwa zaidi ya ule ambao alikua analipwa na Al Ain ambapo alikua analipwa £163,000. Mchezaji huyu mwenye miaka 29 amepokelewa na mashabiki wengi akitegemea kushiriki Chinese Super League.

Club ya Shanghai SIPG inasajili majina makubwa kwa lengo la kupata ushindi kwenye mechi na pia kupata umaarufu ambao wataumia kuiuza brand ya club yao kwenye makapuni mengi ya kibiashara yalipo China. Fursa ya biashara nchini China ni kubwa na ushabiki wa soka upo juu, ndio maana hawasiti kuwekeza pesa za kutosha ili kuzikuza club zao.

a3

a2



Comments