ARDA TURAN SASA NI RASMI MALI YA BARCELONA LAKINI YUPO HATARANI KUTEMWA NA KABLA YA KUICHEZEA HATA MECHI MOJA
Barcelona imefikia            makubaliano na Atletico Madrid  ya kumsajili            kiungo  Arda Turan kwa pauni milioni 29.
          
          
        Mchezaji huyo            mwenye umri wa miaka 28 alikuwa anawaniwa na Chelsea pamoja na            Manchester United, laki Barcelona imekuwa mshindi na            kumsainisha Turan mkataba wa miaka mitano.
          
          
        Hata hivyo            mchezaji huyo hataweza kuichezea Barcelona hadi Januari            mwakani, kutokana na klabu hiyo kupigwa kitanzi cha kusajili            na FIFA kutokana na kashfa ya kusajili vijana wadogo.
          
          
        Katika            makubaliano ya Barcelona na Atletico            Madrid kuna kifungu kinachoruhusu mchezaji huyo kutemwa na            kurudishwa Atletico kabla ya Julai 20 iwapo rais mpya wa            Barcelona hatakubali kuidhinisha usajili.
          
          
        Uchaguzi wa            kumpata rais mpya wa Barcelona utafanyika Julai 18 na iwapo            mshindi hatakubali usajili wa Turan, basi mchezaji huyo            atarejeshwa Atletico Madrid.
          
          
        Na kama hilo            litatokea, Barcelona watapoteza asilimia 10 ya ada waliyoilipa            Atletico.
        Barcelona imetupia              picha na namna Arda Turan atakavyoonekana kwenye jezi yao
        Arda Turan akiwa              uwanjani dhidi ya Athletic Bilbao msimu uliopita
        
Comments
Post a Comment