WAGANDA WAITUPA TAIFA STARS UWANJA MBOVU WA KIVITA



WAGANDA WAITUPA TAIFA STARS UWANJA MBOVU WA KIVITA
Picha ya Uwanja Uganda
Uwanja wa Nakivubo utakaotumika kwa mechi ya Cranes vs Taifa Stars
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
"Uganda Vs Tanzania – 4th July 2015 – Nakivubo Stadium (Agg: 3-0)"
SHIRIKISHO la Soka Uganda (FUFA) limethibitisha kuwa mechi ya pili ya CHAN kati ya timu ya taifa ya Uganda (Cranes) na Taifa Stars itachezwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Vita wa Nakivubo.
"Mechi imebadilishiwa kiwanja. Imepelekwa Uwanja wa Nakivubo. CAF na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wametaarifiwa," amekaririwa Ahmed Hussein, msemaji wa FUFA na mtandao wa michezo wa Kawowo Sports wa Uganda.
Hata hivyo, Uwanja wa Nakivubo una matatizo mengi yakiwamo ya kutokuwa na mfunmo mzuri wa maji (drainage system) hasa wakati wa mvua ambapo mfumo wa maji umeharibiwa na matengenezo yanayoendelea uwanjani hapo.

 



Comments