VIDAL AHUSISHWA TENA NA UHAMISHO WA KWENDA ARSENAL



VIDAL AHUSISHWA TENA NA UHAMISHO WA KWENDA ARSENAL
ARTURO VIDAL ni mchezaji mpya wa Arsenal kwa asilimia 90 baada ya Arsene Wenger binafsi kuruhusu mchakato wa kumpeleka kiungo huyo wa Juventus uendelee.
Arturo              Vidal
ANASAKWA: Arturo Vidal bado anasakwa na Arsenal
Wenger analazimika kutema pauni milioni 21 ili kuweza kupata huduma ya kiungo huyo.

Kwa mujibu wa kituo cha Radio Cadena Cope ya Hispania, staa huyo wa kimataifa wa Chile mwenye umri wa miaka 28, amempiku Morgan Schneiderlin kama lengo la msingi katika orodha ya usajili wa Wenger kiangazi hiki.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Hispania, Wenger analazimika kutema pauni milioni 21 ili kuweza kupata huduma ya kiungo huyo.

Gazeti la The Sun la Uingereza liliripoti Jumatatu asubuhi kuwa Vidal hayuko kwenye rada za Arsene Wenger, lakini sasa inatajwa kuwa Arsenal inajipanga kumpeleka Emirates kiungo huyo aliyekosa kwa ncha kujiunga na Manchester United msimu ulipita.



Comments