VAN GAAL AMWAMURU DE GEA KURIPOTI MAZOEZINI WIKI IJAYO WAKATI MAN UNTED ITAKAPOANZA MAANDALIZI YA MSIMU MPYA




VAN GAAL AMWAMURU DE GEA KURIPOTI MAZOEZINI WIKI IJAYO WAKATI MAN UNTED ITAKAPOANZA MAANDALIZI YA MSIMU MPYA
DAVID DE GEA huenda akalazimishwa kurejea United wiki ijayo wakati klabu hiyo itakapoanza mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya, licha ya kuonyesha kwake kuwa anataka kuondoka Old Trafford.
De Gea anataka kwenda Real Madrid kwa udi na uvumba ili kukamilisha njozi zake za kuitumikia miamba hiyo ya Hispania.
NGOMA NZITO: Safari ya De Gea Real Madrid bado haijanyooka
"Labda tu dili la kipa huyo kwenda Real Madrid likamilike kabla ya timu haijaanza mazoezi Jumatatu vinginevyo De Gea ni lazima aripoti klabuni."
Lakini Daily Star la Uingereza linaandika kuwa boss wa United Louis van Gaal amemwamuru kipa huyo kuwasili mazozeni Jumatatu bila kukosa.
Habari za ndani ya klabu hiyo zimesema: "Labda tu dili la kipa huyo kwenda Real Madrid likamilike kabla ya timu haijaanza mazoezi Jumatatu vinginevyo De Gea ni lazima aripoti klabuni."
De Gea, 24 amekataa ofa ya mkataba mpya United ambao ungemwingizia pauni 200,000 kwa wiki na kumfanya awe kipa anayelipwa pesa ndefu zaidi duniani.
Kwa upande mwingine United nayo imekataa ofa ya pauni milioni 15 ya Real Madrid na kuwaambia kipa huyo ana thamani ya pauni milioni 30.


Comments