VAN GAAL AFUMUA SERA ZA MANCHESTER UNITED ZA MECHI ZA MAJARIBIO KUJIANDAA NA MSIMU MPYA


VAN GAAL AFUMUA SERA ZA MANCHESTER UNITED ZA MECHI ZA MAJARIBIO KUJIANDAA NA MSIMU MPYA

LOUIS VAN GAAL ameufumua utaratibu uliozoeleka wa mwanzo wa msimu wa Manchester United ili kuhakikisha anaanza vema kampeni ya kusaka taji la Premier League.

Manchester United ditch Old Trafford pre-season                friendly
MAGEUZI: Louis van Gaal ameamua kuja kivingine
Bosi huyo wa United ameamua kuachana na mazoea ya  klabu hiyo kucheza mchezo wa majaribio Old Trafford siku chache kabla ya mechi yao ya kwanza ya ligi.
Van Gaal anataka wakae na wiki nzima kabla ya kucheza mechi ya kwanza ya ligi ya ligi kuu.
United itafungua pazia la Premier League dhidi Tottenham ndani ya dimba la Old Trafford, August 8 na haitacheza mchezo mwingine wa kujipima nguvu baada ya mechi yao ya mwisho Julai 30 dhidi ya Paris St Germain huko Chicago, USA.
Van Gaal alisema: "Nimeimba bodi tuachane na mpango wa kucheza mechi wiki moja kabla hatujacheza mchezo wetu wa kwanza wa Premier League.
"Mwaka uliopita tulicheza dhidi ya Valencia siku nne kabla hatujacheza na Swansea City na ikatugharimu, tukadondosha pointi nyingi".
"Kwahiyo imekubalika kuwa hatutacheza wiki moja kabla ya ligi kuanza, mchezo wetu wa kwanza ni muhimu na tunataka kushinda, natumai tutakuwa na mwanzo mzuri."



Comments