Winga wa Manchester United Angel Di Maria, 27, anasakwa na Barcelona (Sport).
Matumaini ya Arsenal kumsajili Jackson Martinez, 28, kutoka Porto yamekwisha baada ya mchezaji huyo kutoka Colombia kusaini mkataba wa miaka minne Atletico Madrid (AS).
Manchester United wanamtaka Sergio Ramos ili kubadilishana na David De Gea. Real Madrid wanamtaka De Gea, 24, pamoja na pauni milioni 20 za kumnunua Ramos. Utd watamzuia De Gea kuondoka iwapo Real watakataa mpango huo (Daily Star).
West Ham hawatomuuza Andy Carroll msimu huu (Sun).
Newcastle wapo katika nafasi kubwa ya kumsajili Charlie Austin, 25 kwa pauni milioni 14. Mchezaji huyo anatakiwa na Southampton, Chelsea na West Ham (Daily Express)
Newcastle na Stoke wanamtaka winga kutoka Ukraine Yevhen Konoplyanka ambaye atakuwa mchezaji huru baada ya mkataba wake kukamilika na Dnipro (Daily Mirror).
Stoke City wanatarajia dau la pauni milioni 8 kutoka Chelsea kumchukua kipa Asmir Begovic, 28, na watataka Victor Moses kuunganishwa katika mkataba huo (Daily Telegraph).
Hata hivyo matumaini ya Chelsea yana wasiwasi baada ya Moses, 24, kusema hana uhakika kama anataka kurejea Stoke alipocheza kwa mkopo msimu uliopita Times).
West Brom wanajiandaa kumfanya Demba Ba, 30, mchezaji anayelipwa zaidi (Birmingham Mail)
West Ham wamekubali mkataba wa pauni milioni 12 kumsajili kiungo wa Marseille Dimitri Payet, 28 (Daily Mail).
Rais wa zamani wa Real Madrid, Ramon Calderon amesema Manchester United watakuwa na "bahati sana" kumsajili Sergio Ramos, 29 (TalkSport).
Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino ana matumaini ya kuwashawishi wachezaji wake muhimu, kwa kumfaya kipa Hugo Lloris, 28, kuwa nahodha na Harry Kane, 21, kuwa naibu nahodha (Daily Mirror).
Winga wa Chelsea Mohamed Salah, 23, anatarajiwa kuwaambia Fiorentina kama atasalia Italia au la, baada ya kuichezea klabu hiyo kwa mkopo msimu uliopita (Daily Telegraph).
Sunderland wametoa dau la zaidi ya pauni milioni 11 kumchukua kiungo wa PSV Eindhoven Georginio Wijnaldum, 24, ambaye anasakwa pia na Newcastle (Guardian).
Manchester United wameacha kumfuatilia Ilkay Gundogan ambaye huenda akasalia Borussia Dortmund wakati Utd wakitafuta kuingo kwingineko (Daily Star)
Uhamisho uliothibitishwa nitakujulisha.
Comments
Post a Comment