STOKE CITY YAITEGA CHELSEA …YAMTAKA VICTOR MOSES ILI KIPA WAO ASMIR BEGOVIC AENDE STAMFORD BRIDGE



STOKE CITY YAITEGA CHELSEA …YAMTAKA VICTOR MOSES ILI KIPA WAO ASMIR BEGOVIC AENDE STAMFORD BRIDGE
STOKE City itahitaji ipewe Victor Moses katika dili lolote litakalohusu uhamisho wa kipa wao Asmir Begovic kwenda kuziba pengo la Petr Cech huko Chelsea.
Jose Mourinho anamwania kipa huyo wa Stoke ili akawe mshindani wa Thibaut Courtois wakati huu ambao Cech anaelekea Arsenal.
Stoke inataka pauni milioni 8 kwa mlinda mlango huyo wa kimataifa wa Bosnia ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake huku akiwa hajaonyesha dalili yoyote ya kusaini mkataba mpya.
Kocha wa Stoke, Mark Hughes anataka kuendelea kuwa na Moses baada ya kung'ara kwenye klabu hiyo aliyoichezea kwa mkopo msimu uliomalizika.
Chelsea ambayo pia inamtupia macho kipa mkongwe wa QPR Robert Green, iko tayari kumuuza Moses baada ya kumtoa kwa mkopo kwenda Liverpool na Stoke ndani ya misimu miwili iliyopita. 
Victor Moses
MTEGO: Stoke intake kumrejesha Moses Britannia Stadium 
Moses angependelea kubakia Britannia Stadium ambako ana uhakika wa namba ya kudumu kwenye kikosi cha Mark Hughes.


Comments