Sergio Ramso ameiambia Real Madrid kuwa anataka kujiunga na Manchester United kiangazi hiki.
United ilipeleka ofa ya pauni milioni 28.5 kwa beki huyo wa kimataifa wa Hispania wiki iliyopita, lakini ikapigwa chini na Real Madrid.
Hata hivyo baada ya kufahamu juu ya ofa hiyo, Ramos akaweka wazi kwa Real Madrid kuwa anataka kwenda United na kuwaomba wafanye hima ili safari yake ya Old Trafford ifanikiwe.
Ramos ana kipengele cha manunuzi cha pauni milioni 142 kwenye mkataba wake, lakini anaamini ofa hiyo ya United inaendana na thamani halisi ya mchezaji wa umri wake na hasa kwa kuzingatia kuwa amebakiza miaka miwili tu katika mkataba wake.
Ramos amesisitiza kuwa anataka kwenda Old Trafford na kusema kuwa ni United pekee anayotaka Real Madrid ijadiliane nayo.
Sergio Ramos ameiambia Real Madrid kuwa anataka kujiunga na Manchester United
Ofa ya kwanza ya pauni milioni 28.3 kwa Ramos mwenye umri wa miaka 29 ilipigwa chini na Madrid
Comments
Post a Comment