SASA NI VITA YA BARCELONA, MAN CITY NA PSG KWENYE KUSAKA SAINI YA POBGA ...rais mtarajiwa wa Barcleona asema lazima kieleweke
Mgombea urais wa Barcelona JOAN LAPORTA ametumia jina la Paul Pobga kama moja ya kampeni zake.
Laporta amesema kama atafanikwa kuwa rais wa Barcelona kwa mara nyingine tena, basi atahakikisha Pobga anakuwa mchezaji wa kwanza kusajaliwa chini yake.
Mabingwa hao wa Ulaya hawaruhusiwi kufanya usajili hadi mwezi Januari 2016, lakini Laporta anayetegemewa kushinda uchaguzi, anataka kufanya usajili wa awali kwa kiungo huyo wa Juventus na Ufaransa ili kuzipiga bao Manchester City, Real Madrid na Paris St-Germain.
Inadaiwa mabosi wa City wamepeleka ofa ya pauni milioni 65 kwaajili ya kupata saini ya Pobga baada ya kumfanya chaguo lao kuu la usajili wa kiangazi hiki.
Comments
Post a Comment