Nyumba ya David De Gea imewekwa sokoni katika kipindi hiki ambacho inaaminika kipa huyo wa Manchester United yuko mbioni kwenda Real Madrid.
Mmiliki wa nyumba hiyo anayoishi De Gea ameamua kuliuza jumba hilo la kifahari lenye vyumba sita vya kulala akifahamu wazi kuwa mteja wake hatalitumia tena msimu ujao.
Kwasasa zinahesabiwa siku tu kabla De Gea hajajiunga na Real Madrid katika dili ambalo linaweza likamshuhudia sentahafu wa Real Madrid Sergio Ramos akihamia Manchester United.
Jumba la vyumba sita la De Gea huko Cheshire limewekwa sokoni ikiwa ni dalili kuwa safari yake ya Real Madrid imeiva
Mmiliki wa jumbo analoishi De Gea ameamua kulipiga bei
Upande mwingine wa nyumba De Gea inavyoonekana
Sehemu ya ndani ya mjengo anaoishi De Gea
De Gea akiwa na mchumba wake Edurne Garcia
Sehemu nyingine ya ndani ya mjengo wa De Gea
Eneo la bafuni linavyoonekana
Sergio Ramos (kulia) huenda akahamia Manchester United
R
Comments
Post a Comment