ROY KEANE ASEMA KAMA MITANDAO YA KIJAMII INGEKUWEPO ENZI ZAO BASI ANGEISHIA JELA ...adai mazoezi ya Man United yalikuwa na ushindani kuliko mechi za Premier League
Nahodha wa zamani wa Manchester United, Roy Keane ameponda maisha ya sasa ya wanasoka ambao wengi wanakesha kwenye mitandano ya kijamii.
Roy Keane anasema kama kama mitandao hiyo ingekuwepo enzi zake za uchezaji soka basi angeishia jela.
"Kama kungekuwa na mitandao ya kijamii enzi zangu, basi ningeishia jela," anasema Roy Keane bila kufafanua.
Kiungo huyo aliyekuwa mtukutu uwanjani anasema enzi hizo mazoezi ya Manchester United yalikuwa yana ushindani kuliko mechi zenyewe.
Wakati wa enzi za Roy Keane miaka ya 90 na mwanzoni mwa 2000, wapinzani wakubwa wa Manchester United kwenye ligi walikuwa ni Blackburn, Arsenal na baadae Chelsea lakini Keane anasema ubora wa kikosi cha United kilipelekea mazoezi yawe na ushindani mkubwa kuliko mechi.
"Jumamosi (siku za mechi) ilikuwa ni kama mapumziko kwetu kwani mazoezi ndio kilikuwa kitu kigumu zaidi," anaeleza Keane aliyeshinda mataji saba ya Premier League na manne ya FA Cup ndani ya Old Trafford.
Keane anasema wanasoka vijana wa siku hizi kila siku utawaona kwenye mitandao ya kijamii wakitupia picha zao za kujirusha, kitu ambacho amedai hakina manufaa yoyote kwenye soka.
Roy Keane alishinda mataji saba ya Premier League katika muda wake ndani ya Manchester Untied
Keane anaemia mazoezi ya Manchester United yalikuwa na ushindani kuliko mechi zenyewe
Keane akizungumza na shabiki aliyevalia jezi ya Ireland
Keane na Patrick Viera wa Arsenal walikuwa wapinzani wa jadi lakini Roy Keane bado anasema mazoezi ya United yalijaa ushindani kuliko mechi za ligi
Comments
Post a Comment