Nyota wa zamani wa Barcelona Ronaldinho na Samuel Etoo huenda wakaungana tena kukupiga pamoja kwenye klabu ya Antalyaspor ya nchini Uturuki.
Wiki iliyopita Antalyaspor ilitangaza kwamba, taryari imefikia makubaliano ya kumsajili Eto'o, 34, kutoka klabu ya Sampdoria ya nchini Italia.
Sasa wamesema wamefikia makubaliano ya kumsajili mchezaji mwenzake wa zamani Ronaldinho ambae walikipiga pamoja kwenye klabu ya FC Barcelona baada ya mkataba wake na klabu yake ya Queretaro ya Mexico kuvunjwa.
Umit Akbulut ambaye anamuwakilisha Ronaldinho nchini Uturuki amesema, ameshakutana na kakayake Ronaldinho na Rais wa Antalyaspor Gultekin Gencer na tayari wameshafikia makubaliano juu ya dili hilo.
Akbulut ameongeza kuwa, klabu hiyo ya Uturuki ilikuwa imepanga kuwatambulisha Ronaldinho na Eto'o kwa pamoja Julai 7.
Aliposti pia video ya Ronaldinho kwenye account yake ya Instagram ambayo inamuonesha mchezaji huyo ambaye aliwahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara mbili akisema: "Hivi karibuni nitakuwa Uturuki".
Ronaldinho ambaye alicheza Barcelona sambamba na Eto'o kati ya mwaka 2004 na 2008, anahusishwa pia kujiunga na klabu ya Vasco da Gama ya nchini kwao Brazil.
Comments
Post a Comment