Real Madrid wamekumbwa na hofu ya kumpoteza Sergio Ramos licha ya kukataa ofa ya paundi milioni 35 kutoka kwa Manchester United.
Inafahamika kwamba Rais wa Real Madrid, Florentino Perez ameamua kumuita Ramos katika mazungumzo binafsi na anataka kumhakikishia kwamba matatizo kuhusu mkataba wake yataisha baada ya kurudi kutoka kwenye likizo yake huko America na kabla ya Rafa Benitez kuondoka na kikosi Julai 11 mwaka huu kwenda Australia na China kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya kila kitu kitakaa sawa.
Hata hivyo, Real wameendelea kuhofia kwasababu Ramos tayari ameonesha kutaka kuondoka baada ya kukaa miaka 10 Bernabeu.
Habari mbaya kwa United ni kwamba, Real wamefikiria kupandisha dau mpaka paundi milioni 65 ili kuwazuia wazee wa Old Trafford kuinasa saini ya mlinzi huyo kisiki.
Comments
Post a Comment