REAL MADIRD YAANZA KUHOFIA KUWA ITAPOTEZA UWEZO WA KUMZUIA RAMOS KWENDA MANCHESTER UNITED ...yamweka sokoni kwa pauni milioni 65



REAL MADIRD YAANZA KUHOFIA KUWA ITAPOTEZA UWEZO WA KUMZUIA RAMOS KWENDA MANCHESTER UNITED ...yamweka sokoni kwa pauni milioni 65
Real Madrid imeanza kuhofia kuwa inapoteza uwezo wa kumzuia Sergio Ramos asiondoke licha ya kuipiga chini ofa ya pauni milioni 35 ya Manchester United.
Rais wa Real Madrid Florentino Perez alichukua hatua ambayo si ya kawaida ya kuwasiliana na Ramos na kumwambia mkataba wake utashughulikiwa pindi mchezaji huyo akirejea klabuni kutoka likizo yake huko Marekeani kabla kikosi cha Rafa Benitez hakijaondoka Julai 11 kwenda Australia  na China kujiandaa na msimu mpya.
Lakini Real Madrid inaendelea kutatizwa na namna mchezaji huyo alivyosisitiza kuwa anataka kuondoka baada ya uwepo wake wa miaka 10 na sasa klabu hiyo imeamua kuweka kiwango cha pauni milioni 65 kwa klabu itakayotaka kumnunua.
United imeamua kutenganisha mjadala wa Ramos na De Gea na watataka walipwe pauni milioni 35 ili kipa huyo wa Hispania aende Real Madrid.
Katika hili, maofisa wa Old Trafford hawajali kuwa De Gea amebakiza mwaka mmoja tu wa mkataba wake, wanachotaka wao ni pesa ndefu vinginevyo bora aondoke bure kiangazi kijacho.
Real Madrid have rejected                    Manchester United's opening offer of £35million for                    centre back Sergio Ramos
Real Madrid ilikataa ofa ya  Manchester United ya £35 million kwaajili ya Sergio Ramos
Ramos looks to be on his                    way out of La Liga giants Real Madrid, with United                    considering a revised offer
Ramos amesema anataka kuondoka Real Madrid
The Spaniard wants his                      future resolved by the time he returns on July 10                      for Real's pre-season training tour
Mchezaji huyu wa kimataifa wa Hisapania anataka Madrid wamalizane nae kabla ya Julai 10
United are still to                      receive a bid from Madrid for David de Gea but are                      determined to strike a decent deal
Madrid nao wanamtaka De Gea lakini United imetingisha kibiriti




Comments