PETR CECH: TOMAS ROSICKY ALINISHAWISHI KUONDOKA CHELSEA NA KUJA ARSENAL



PETR CECH: TOMAS ROSICKY ALINISHAWISHI KUONDOKA CHELSEA NA KUJA ARSENAL

PETR CECH amefichua kuwa maongezi yake na nyota mwenzake wa Jamhuri ya Czech, Tomas Rosicky, yamechangia kumshawishi kujiunga na Arsenal.
Cech, 33 amekamilisha usajili wake wa Arsenal siku ya Jumatatu kwa pauni milioni 10 baada ya kushinda  mataji 15 katika miaka yake 11 aliyoitumika Chelsea.
Hata hivyo ujio wa kipa Thibaut Courtois ukamfanya apoteze namba Chelsea na kuwa chaguo la pili, hali iliyomfanya afikirie kutafuta changamoto nyingine, huku Rosicky  akiwa chachu ya safari hiyo ya Arsenal.
Tomas Rosicky convinced Petr              Cech to hold talks with Arsenal
NYOTA WA CZECH : Tomas Rosicky (kushoto) alimshawishi Petr Cech kuhamia Arsenal
"alinieleza mengi mazuri juu ya Arsenal"
Petr Cech
"Ndio tulikuwa tukiongea - mara nyingi tumekuwa na muda wa kukaa pamoja kwenye timu ya taifa, lakini wakati huo sikujua nini kingetokea," anaeleza Cech.
"Lakini Rosicky alionekana mwenye furaha na aliyependa kuichezea Arsenal siku zote, alinieleza mengi mazuri juu ya Arsenal, alikuwa ni moja ya sababu iliyonifanya nichague Arsenal"


Comments