HUGO LLORIS amekubaliana kwa mdomo na Mwenyekiti wa Tottenham Hotspur, Daniel Levy kwamba atauzwa kama itatokea ofa ya pauni milioni 17.8 au zaidi.
Gazeti la L'Equipe la Ufaransa limeripoti kuwa makubaliano kati ya kipa huyo Mfaransa na mfanyabiashara huyo, yalifikiwa mwaka jana wakati aliposaini nyongeza ya miaka mitano katika mkataba wake.
Kipa huyo wa Tottenham yupo kwenye listi ya Manchester United kama Real Madrid itaweza kufika bei ya kumtoa David De Gea Old Trafford.
Lloris – kipa namba moja wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 28, ana nia ya kucheza Champions League na kikosi cha Louis Van Gaal kitaanza kushiriki michuano hiyo katika hatua ya mtoano mwezi Agosti.
Mfaransa huyo alihamia White Hart Lane kwa pauni milioni 11.4 kutoka Lyon – kikosi ambacho kilimtumia katika Champions League mwaka 2012.
Comments
Post a Comment